THE HISTORY OF TANDALA TEACHER COLLEGE
Chuo cha Ualimu Tandala kilianzishwa mwaka 1975 na kiko katika Wilaya ya
Makete Mkoa wa Njombe. Chuo kipo umbali wa kilometa 85 kutoka makao makuu ya Mkoa
na kilometa 30 kutoka makao makuu ya Wilaya. Chuo hiki kilianzishwa kwa
madhumuni ya kutekeleza Agizo la Musoma lililohusu kufikiwa
kwa Elimu
kwa Wote (UPE) ifikapo mwaka 1977. Chuo kilirithi majengo ya iliyokuwa
Shule ya Kati (Middle School) iliyokuwa ilimilikiwa na Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kusini Kati, kutokana na mahitaji ya walimu
yaliyosababishwa na ongezeko la wanafunzi wa shule ya msingi kanisa kwa hiari
yake lillitoa majengo ya shule hiyo kwa lengo la kuanzisha mafunzo ya Ualimu.
Mafunzo ya Ualimu ambayo yamekuwa yakitolewa
tangu Chuo kilipoanza ni pamoja na Daraja la IIIC (1975 – 1985), Daraja la IIIB
(1985 – 1996), Daraja la IIIA (1994 – 2015), mafunzo ya Walimu kazini
kuanzia daraja la CB hadi A (MUKA) kuanzia 2004 hadi 2007. Kwa sasa Chuo
kinaendesha Programu mpya ya Mafunzo ya Walimu kwa Ngazi ya Diploma.
0 comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.